Suki ni mwanafunzi wa darasa la sita. Alikuwa akijiwekea akiba ili anunue kitabu cha picha za wanyamapori wakati wa likizo. Kabla ya siku ya kwenda kununua kitabu kufika, tukio la ajabu linatokea. Mwizi anaingia nyumbani kwa kina Suki na kuiba kisanduku cha Suki cha kuhifadhi pesa na vitu vingine. Askari polisi wanaarifiwa kuhusu wizi huo, lakini hawafanikiwi kumkamata mwizi. Suki anaamua kufanya upelelezi ili ajue ni nani aliyeiba kisanduku chake. Je, atafanikiwa?
Creation date: 2017-10-31
30 Pages