Silaha 100 za Kiongozi, ni silaha za aina ya pekee na ni maalumu. Hizi ni tofauti kabisa na silaha tulizozoea kuziona au kuzisikia. Silaha hizi zimetengenezwa ili zimsaidie kiongozi kumlinda dhidi ya mashambulizi kutoka kwa “maadui” wake. Katika kitabu hiki, neno Kiongozi, linajumlisha viongozi wa familia, siasa, serikali, dini, kazi, ushirika, taasisi za serikali, asasi zisizo za serikali, asasi za serikali, mashirika ya umma, makampuni na wengine. Viongozi hawa wote wanapigwa vita vya kila namna, kwa hiyo, ili waendelee kuongoza, wanahitaji kuwa na silaha za kujilinda. Vita hivi vinatoka kwa viongozi wenzao, kwa watu wanaowaongoza na hata watu wasiowaongoza. Vita vipo na ni vya kweli. Asipopigana kwa kutumia silaha hizi atashindwa vita hivyo.
Creation date: 2018-08-10